Duration 3:29

WAZIRI MALIASILI NA UTALII AWAPA MIKAKATI YA UHIFADHI WAHIFADHI MISITU, WATAKAOKAIDI KUPOTEZA AJIRA

1 573 watched
0
7
Published 5 May 2021

"Nihitimishe hotuba yangu kwa kuwakumbusha kuwa ni wajibu wenu kufanya kazi kwa kuepuka vishawishi vinavyoweza kuwa chanzo cha rushwa na migogoro katika usimamizi wa misitu nchini," Waziri Maliasili na Utalii. Wakati wote hakikisheni kuwa; i. Mnapanga shughuli zenu kwa kushirikiana kwanza na watumishi wenzenu na pia taasisi nyingine katika ngazi zenu za wilaya; ii. Mnasimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu zote bila upendeleo wa aina yeyote; iii. Mnapiga vita na kujiepusha na rushwa katika maeneo yetu; iv. Mnatumia mifumo ya kielekronic iliyobuniwa na serikali katika kukusanya na kutumia fedha za umma kikamilifu; v. Mnakusanya mapato ya serikali na kuzuia mianya yote ya upotevu katika maeneo yenu; vi. Mnakuwa wadau wa kwanza kuepusha migogoro baina ya hifadhi za misitu na watumiaji wengine katika maeneo yenu; vii. Muwe kiungo cha utendaji na wadau wengine kama NGOs zinazotekeleza miradi na wakati wote kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo unaleta mazingira ya uendelevu wa misitu (sustainability)

Category

Show more

Comments - 0