Duration 6:28

Je Kimo cha Tumbo hufanana na Umri wa Mimba | Je lini Urefu wa Tumbo hufanana na Umri wa Ujauzito.

7 830 watched
0
69
Published 10 Oct 2021

Kwa kawaida Urefu au Kimo Cha Tumbo huanza kupimwa Mimba inapofikisha wiki 20 kwenda katika kipindi cha Ujauzito. Lakini Uwiano Kati ya Umri wa Mimba au Ujauzito katika wiki huwiana ipasavyo na Urefu wa Tumbo au Kimo Cha Tumbo Mimba inapofikisha Wiki 20 hadi 32, ina maana zaidi ya Wiki 32 Mtoto anaweza kuwa ameshuka na Urefu ukawa hauwiani na umri wa Mimba. Urefu wa Tumbo au Kimo Cha Tumbo Mara baada ya kupimwa huweza kuwiana na umri wa Mimba endapo tuu Urefu huo hautakuwa pungufu au zaidi ya 3cm. Mfano; 1. Endapo una Mimba ya umri wa Wiki 20, Urefu wa Tumbo ukiwa kati ya 17cm,18cm,19cm,20cm,21,22 na 23cm huwa inaonesha kuwa kuna Uwiano Kati ya Umri wa Mimba yako na Urefu au Kimo cha Tumbo. 2. Endapo una Mimba ya Wiki 25 ina Ina Urefu wa Tumbo hutakiwa kuwa Kati ya 23cm hadi 28cm. 3. Endapo una Mimba ya Wiki 28 ina Ina Urefu wa Tumbo hutakiwa kuwa Kati ya 25cm hadi 31cm. KUMBUKA: Unapopimwa Urefu au Kimo Cha Tumbo katika kipindi cha Ujauzito huweza kusaidia kujua ukuaji wa Mtoto kulingana na Umri wa Mimba yako vile vile huweza kusaidia kujua Uwingi wa Maji yanayomzunguka Mtoto katika Mji wa Uzazi. #drmwanyika #mamaafya #KimoChaMimba

Category

Show more

Comments - 138