Duration 2:00

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAIPONGEZA NHC

138 watched
0
3
Published 17 Sep 2021

Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Shaka Hamdu Shaka, leo tarehe 17/9/2021 ametembelea mradi unaotekelezwa na NHC wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara. Akiwa katika ziara hiyo, Ndugu Shaka amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kinatambua kazi nzuri inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala. Hivyo, kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kazi nzuri ya kupigiwa mfano ya ujenzi wa jengo hilo la kisasa litakalosaidia kupunguza gharama kwa Wananchi wa Kanda ya Kusini za kufuata huduma ya matibabu ya ngazi ya rufaa Jijini Dar es salaam. Amesema kuwa kwa miaka mitano iliyopita NHC imekuwa ni kimbilio kubwa la Chama cha Mapinduzi katika utekelezaji mahiri na makini wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuliunga mkono Shirika la Nyumba la Taifa ili liweze kusaidia Watanania wengi zaidi.

Category

Show more

Comments - 1